Prayer
His Majesty's Worldwide Prayer Sanctuary is available to you 24-hours-a-day. His Majesty invites you to partake of His mercy and grace through our audio prayers of agreement available in our Prayer Sanctuary, or feel free to e-mail us your prayer petitions and allow our Worldwide HMM Intercessors to take them to the throne room of God. His Majesty's line is never busy and all prayer requests are confidential!
Do You Know Jesus?
For God so loved the world, that He gave His only begotten Son, that whosoever believeth in Him should not perish, but have everlasting life. (John 3:16)
Archives

His Majesty Ministries Prayer Of Agreement and Communion - Africa

Written by Sharyn Culp
Translated by George Imbera, Africa HMM Director
Inspired by Holy Spirit

(Beloveds, this is the Prayer Of Agreement the HMM Worldwide Prayer Sanctuary Intercessors pray once weekly meeting in the Spirit establishing God's Kingdom come, His will be done on earth, as it is in heaven worldwide (Matt. 6:10; Zech. 4:6). After we pray we seal our prayers with the blood of Jesus partaking of Communion together believing "it is finished" in Jesus' name. Amen. We invite you to join us and bless you knowing the Lord will not forget to reward you for your labors of love towards Him, His Kingdom and His Majesty Ministries (Heb. 6:10). 

Maombi ya mahala patakatifu kote ulimwenguni ya huduma wa utukufu wake Maombi ya Upatanisho

Baba ni katika jina la Yesu, tunakushukuru na kukusifu kwa kuwa wewe ni Mungu wa miujiza. Pia tunakushukuru na kukusifu kwa kuwa wewe ni Mungu wa urejesho. Tunakushukuru na kukusifu kwa kuwa wewe ni Mungu mwenye nguvu na pia Alfa na Omega, Mungu aliye kati ya mwanzo na mwisho. Twashukuru kwa damu ya yesu Kristo, neno lako na roho mtakatifu. Twakushukuru tunapokuja kwako kupitia kwa maombi haya ya upatanisho tunapoelekeza imani yetu katika kitabu cha Mathayo 16: 18 na Mathayo 18:18 – 20 pamoja na Huduma ya Utukufu wako. Unatusikiliza na kutupa majibu kabla hatujatia kikomo kuongea kama jinsi ilivyo katika Isaya 65:24. Baba, ulisema katika neno lako, kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 7:14 "Kama watu hao wangu wakijinyenyekesha,wakasali, wakanitafuta na kuacha njia zao mbaya, basi mimi nitawasikiliza kutoka juu mbinguni nitawasamehe dhambi zao na kuistawisha nchi yao". Kwa wakati huu Baba, kwa utiivu wa neno lako, sisi watu wako tulioitwa kwa jina lako,twanyenyekea kwa kutubia makosa ya Israeli, Marekani, Mataifa ya ulimwengu, mwili wa kristo, unganiko la Marekani, Huduma ya Utukufu wako, kila mwombezi anayepatana pamoja nasi katika maombi akiwa pamoja na jamii ya wapendwa wake, na kwa niaba ya maombi yanayotumwa na kupokelewa na Huduma ya utukufu wako. Tunaomba msamaha wako tukaweze kugeuka na kuziwacha njia zetu mbaya, tunapoamini unatusikiliza kutoka mbinguni, ukitusamehe dhambi zetu na kuponya nchi yetu na ulimwengu wote kwa jumla. Katika jina la yesu, tunamuita shetani mwizi na tunateka nyara na kurejesha milki zote ambazo shetani aliiba kutoka Israel, Marekani,mataifa yote,mwili wa kristo, unganiko la Marekani,huduma wa utukufu wako, kila mwombezi anayepatana pamoja nasi katika maombi akiwa pamoja na jamii ya wapendwa wake, na kwa niaba ya kila ombi linalopokelewa na huduma ya ufalme. Tunateka nyara kila milki tukirejesha kwako Ufalme kwa nguvu huku tukidai makundi saba ya urejesho wa kila kitu ambacho shetani alimuibia mtakatifu na ufalme wake pamoja nasi. Watoto wa mfalme kama ilivyo katika Mathayo 11:12 na Mithali 6:30-31. Kwa upatinisho twasimama kwa pengo kwa kutangaza vita mbinguni na kukemea na kuchukua mamlaka kutoka kwa shetani na kwa kila pingamizi,kila nguvu, kila mtawala wa giza na kuangusha chini roho zote za uzinifu kutoka mahali pa juu zilizo kinyume na milki hizii kulingana na Wakorintho wa Pili 10:4-5. Katika jina la yesu tunafuata kila neno lililo nenwa kinyume na milki hizi na kuomba msamaha kwa wote walionena kinyume na pasiwe na nguvu zozote zitakazofanya kazi twazionya na kuzifuta na damu ya yesu kristo kwa upatanisho twafutilia mbali mipango yote iliyokuwa imepangwa juu ya milki hizi na kuitangaza kushindwa kufanya kazi katika jina kuu la yesu Kristo, na katika Isaiya 54:17. Tunaharibu na kugeuza laana zote juu ya milki hizi katika jina la yesu kristo, na katika Wagalatia 3:13 tunalihimidi jina la yesu kristo juu ya milki hizi tunalihimidi na kuyafunika mataifa haya kwa nguvu za kipekee za yesu kristo. Tunanena, tunalihimidi, na kukiri neno la Mungu juu ya mataifa haya. Tunakemea muovu aharibuye na aondoaye roho mtakatifu juu ya mataifa haya katika jina la yesu kristo. Tunatangaza sasa kulingana na Mathayo 6:10 ufalme wa utukufu wako uje, mapenzi yako yatimizwe, dunaini kama yalivyo mbinguni na yatimike Israeli, Marekani, mataifa yote, mwili wa kristo , unganiko ya Marekani huduma wa utukufu wako katika maisha ya kila mwombezi ambaye anaunganika nasi katika maombi pamoja na wapendwa wa jamii yake na kwa niaba ya kila maombi yanayopokelewa na utukufu wako, tunasema yote yamefanyika kwa imani tukiwa tunatarajia kuona majibu ya utimilifu wako wote kwa mambo tunayokuulizia katika maombi, tunakushukuru na kukusifu ewe mtakatifu kwa kuheshimu imani yetu, damu yako, maombi yetu ya upatanisho na kwa neno lako ndani ya jina la yesu Amen. Haki ya uchapisho@ 2002 Huduma ya utukufu wake Inc. Wapendwa vifungu vya ushirika na roho mtakatifu vimenakiliwa hapo chini kwa ufasaha wako. Maana kila mnapokula mkate huu na kunywa kikombe hiki mwatangaza kifo cha Bwana mpaka atakapokuja kwa hiyo kila mnapokula mkate huu na kunywa kikombehiki mwatangaza kifo cha bwana mpaka atakapokuja. Kwa hiyo kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya bwana. Basi kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza ndipo ale mkate huo na anywe kikombe hicho. Maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili na Bwana, anakula na kunywa hukumu yake yeye mwenyewe. Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa na wengine kadhaa wamekufa. Kama tungejichunguza wenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo (1Wakorintho 11:27 – 33). "Akamshukuru Mungu, akaumega, akasema, huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa kunikumbuka vivyo hivyo, baada ya kula akatwaa kikombe cha divai akasema, hiki ni kikombe cha agano jipya linalodhibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi kila mnapokunywa kwa kunikumbuka" (1Wakorintho 11:24 – 26) Aliye mtukufu anawapenda.

©2002-2002 His Majesty Ministries 

 

© 2010 - 2024 His Majesty Ministries Worldwide Inc - All Rights Reserved.